Monday, August 17, 2009

LEILA ABDULL AMETUTUMIA MAKALA HII JUU YA MAISHA YA UGHAIBUNI, HEBU IPITIE MDAU....

Kwa wengi wetu hapa ambao tunakaa nje ya Tanzania, iwe Japan, Russia,Finland, US, UK, SA, Malaysia, France, Swiss, Ujerumani, Brazil,Canada na nchi zingine za ulimwengu wa kwanza au wa pili, si siri kuwachimbuko la maendeleo yao halikuwa katika sera pekee, hotuba au hatakama tukidai ni matunda ya ukoloni na utumwa (unyonyaji), bali nikutokana na uchapakazi ulioambatana na ufanisi, uvumbuzi, tija namaarifa.Kwa wastani, Wamarekani wa middle class. huwa wanafanya kazi takribanmasaa 50-60 kwa wiki. Wale wa KCC ndio huvuta dabo shifti, kazi tatuili kujikimu na hawa hufikia hata kufanya kazi kati ya masaa 80-100kwa wiki.Hata matajiri au tabaka la juu, nao ni wachapa kazi na wao maranyingine hupita hata masaa 100 kwa wiki wakiwa katika kuhamasishauzalishaji mali, kupelekeshana puta na uvumbuzi hata ufanisi, iliwaendelee kuwa tabaka la juu na kuendelea kuwa na ongezekop marudufula kipato (utajiri).Nitatoa mfano wa Warren Buffet, tajiri kuliko wote duniani. AnakaaOmaha, anaamka saa 10 asubuhi, baada ya kupiga tizi, anakimbiliamagazeti kabla ya kuanza mikutano na wafanyakazi wake, matajiriwenzake au kwenda kazini kwenye shughuli 100 ambazo huishia kwendakulala saa 4 hadi saa 5 usiku, kisha siku mpya huanza tena saa 10asubuhi, hivyi kuwa na mzunguko wa kufanya kazi.Mtu wa kima cha chini Jane/Jone Doe, huamka saa 10 asubuhi, nakuondoka nyumbani kwake baada ya kumuacha mwenza aangali watoto kablaya kwenda shule. Nitamtumia Jane/John Doe ambaye kazi yake nikusafisha ofisi, dereva wa basi, mpishi au mlinzi. Kazi anaanza rasmisaa 12 asubuhi au mapema, hufanya kazi kwa masaa 8 kisha huenda kwenyekazi nyingine ambayo anaingia saa 10 jioni na huko hufanya kazi kwamasaa 5 kabla ya kwenda nyumbani hoi bin taabani, kulala na kuamkamapema tena siu inayofuata.Mimi huamka saa 12 asubuhi, natakiwa kazini saa 2 asubuhi, kila siku
hutoka kazini kurudi nyumbani kati ya saa 1 hadi saa 3 usiku. Mudawangu wa kwenda lunch ni saa 1. Huingia kitandani saa 5 au 6 usiku(pamoja na kuleta kazi nyumbani kumalizia kiporo. Kisha huamka tenasiku inayofuata asubuhi na mapema kuanza sakata jipya.Kwa wastani, Mmarekani au wale wanaoishi marekani hufanya kazitakriban si chini ya masaa 12 kwa siku. Kuna wanaolipwa kwa saa, nakuna wanaolipwa mshahara bila kujali masaa.Ikiwa mimi nalipwa mshahara bila kujali masaa na kwa wastani nafanyakazi karibu masaa 50-60 kwa wiki na wale direct reports wanguwanaofanya kazi kwa kulipwa ujira wa saa nao hufanya kazi na mimi(huenda wana kazi nyingine za ziada) kwa masaa 40 ya kwanza na yaleyote ya ziada ni OT, najiuliza, je ni ajabu kuwa wenzetu kama Taifakwa kupitia viwanda, na hata shughuli za huduma mpaka kilimowanaendelea kuitwa nchi zilizoendelea?Ikiwa kuchapa kazi bila kubangaiza ndio tabia na utamaduni waMmarekani, Mchina, Mjapan hata Mbrazil, je sisi Watanzania tunautamaduni na tabia gani mbele za kazi?Nakumbuka nikifanya kazi nyumbani (TZ), kwanza ukichelewa kazini(unatakiwa kazini saa 2 asubuhi), unalaumu Uda na vipanya, ukishaingiana kuonekana, unatoweka kwenda kupata kifungua kinywa, unapotea kwamuda wa nusu saa hadi saa kamili (unalipwa kwenda tafuta kifunguakinywa!), mchana ukiwadia, Lunch ni saa moja na ushehe, kisha saa tisaalasiri kuna kupata kitafunwaji kingine, ikifika saa kumi jioni, nikufungasha makabrasha haraka kuwahi basi la kukurudisha nyumbani aukukimbilia "stoo" kwa mama vitunguu kuziguguda!Ukiangali kwa watsani, muda niliofanya kazi ni masaa 5.5-6 na mawilikatika hayo masaa 6 ni kubangaiza kwa stori za mpira, wanawake, siasa,kupekenyua Dar Hotwire na kupanga mikakati ya kilauri!Najiuliza leo hii, pamoja na kuwa twadai nidhamu ya kazi imerudi (kwawale wanaofanya kazi kwenye makampuni binafsi na ya kigeni!), lakini
tija na ufanisi wetu ni bado unagota, tunatarajiaje kuwa tutapigahatua?Kukitokea msiba kwa jirani, twachukua siku tatu (tena unalipwamshahara!) kuomboleza, Ng'ombe akikata kutoa maziwa, twaenda kazini nakuaga "nakwenda kwa veti" huku muda ambao haupo, unaendelea kulipwa,mbaya zaidi, tunataka mwajiri atulipie huduma za afya, nauli ya basina lanchi!Jee tutafika na kufanikiwa ikiwa tumejijengea hii tabia ya kuwawabangaizaji na wavivu?Hivi leo wengine waishio nje ya nchi wakirudi nyumbani wakapewa nafasiya kuongoza na waanze kuongoza na kufanya utendaji kama walivyojifunzahuko waliko uchapakazi wa kuhenyeka na ufuatiliaji makini si Tanzaniaitaanza badilika na hasa kama tutakwenda Serikalini (kisingizio kikuucha nchi kukosa maendeleo kila siku ni eti Serikali mbaya!) na kuanzakupaa kwa mwendo wa Kipanga na sii kasungura?Au tukija na hizi tija za "kinyamwezi" kuchapa kazi na kutakauwajibikaji wa kuchapa kazi tutaitwa "wazungu" na kuendewa Bagamoyo auMpanda ili tufundwe? Au vijembe vya chini chini kama vile vilivyompata yule mkuu wa TPRI Dr. Bamwenda au yule Kaburu wa MuhimbiliTrigonometry vitatukumba na kutufanya tuachie ngazi na kutafuta nauli kurudi "utumwani" unyamwezini ambao juhudi za kufanya kazi kwetu zinaheshimika?Hivyo basi ni nini kinatakikana katika kujenga utashi wa Mtanzania awe na jitihada na uchacharikaji kama Mchaga au Mpemba katika utafutaji nakuchapa kazi?

No comments:

Post a Comment