Monday, August 17, 2009

MWANASIASA WA WIKI:KINGUNGE


Kuanzia weekend hii,BC inapenda kutambulisha ukurasa mpya.Huu utakuwa ukurasa wa wanasiasa.Kila jumamosi,tutakuwa tukimuweka na kumjadili mwanasiasa mmoja ambaye katika wiki inayokuwa inaaga,amekuwa akigonga vichwa vya habari aidha kwa mambo mazuri ya kujenga au hata mabaya. Kama ni mazuri atastahili sifa, kama ni mabaya ataambiwa ukweli,ataonywa. Kutakuwa pia na nafasi ya kupiga kura za kijamii ili kupata picha pana na mtazamo wa wananchi kuhusiana na suala husika.

Hii itakuwa nafasi nzuri kwako wewe msomaji,mtembeleaji na mchangiaji wa BC kutoa mawazo yako juu ya mwanasiasa,alichokisema,alichokifanya au sera anazozipigia upatu.

Kwa kuanza leo tunaye mwanasiasa mkongwe,Kingunge Ngombale Mwiru. Bila shaka umefuatilia kwa makini malumbano yanayoendelea baina ya mwanasiasa huyo mkongwe na viongozi wa Kanisa Katoliki kufuatia kupinga kwake Waraka wa Kanisa Katoliki.

Kimsingi lilichokuwa likijaribu kufanya kanisa katoliki ni kutoa elimu kwa waumini wake kuhusiana na sifa ambazo inabidi mtu awe nazo ili apate kuchaguliwa. Bila shaka kanisa linakuwa linalenga kuamsha hisia za wananchi na hususani waumini wa kanisa hilo lenye wafuasi wengi kutokana na ukweli kwamba mwakani ni mwaka wa uchaguzi nchini Tanzania.

Kingunge yeye anadai kuunga mkono Waraka huo wa Wakatoliki ni kama kuachana na ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Je unadhani nani yupo sahihi katika suala hili? Je kanisa katoliki limekosea kutoa waraka au muongozo huo kwa waumini wake? Kingunge Ngombale Mwiru(pichani).Huyu ndiye mwanasiasa wetu wa wiki hii

No comments:

Post a Comment