Thursday, November 5, 2009

Buriani Mzee Alex Kusaga

Mwenyekiti Mtendaji wa Clouds Media Group,Bw Alex Kusaga(Pichani)ambaye ni baba mzazi wa Joseph Kusaga,amefariki jana jioni(Pretoria)nchini Afrika ya Kusini ambako alipelekwa kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa kansa.
Taarifa Za Uhakika zinasema kwamba Msiba wa Mzee Alex Kusaga Upo Nyumbani kwake Mbezi-Beach karibu na Giraffe Hotel jijini Dar es SalaaamMwenyezi mungu Ailaze Roho ya Marehemu mahali Pema Peponi
Amen

MKALIMANI ANATAFUTWA


NATAFUTA MKALIMANI WA KUTAFSIRI KUTOKA KIPOLAND KWEDA KISWAHILI NA AWE ANAJUA KINGEREZA.
KWA MAELEZO ZAIDI TUMA EMAIL KUPITIA,
nganzo88@yahoo.no
SIMU
+4747262181

Agundua Ana Aleji na Mbegu za Kiume za Mumewe Siku ya Harusi


Usiku wa furaha ya harusi uligeuka kuwa usiku wa majonzi baada ya wanandoa kugundua kuwa hawataweza kuwa na uwezo wa kupata mtoto katika maisha yao ya ndoa kwa kuwa bi harusi ana aleji na mbegu za kiume za mumewe.
Mike mwenye umri wa miaka 27 na Julie Boyde mwenye umri wa miaka 26 wakazi wa Ambridge, Pennsylvania nchini Marekani walikuwa katika mapenzi moto moto kwa miaka miwili kabla ya kuamua kufunga ndoa na kuamua kufanya mapenzi bila kutumia kinga kwa mara ya kwanza usiku wa harusi yao.Lakini mambo hayakuenda vizuri kama walivyotarajia kwani ghafla iligundulika kuwa bi harusi alikuwa na aleji na mbegu za kiume za mumewe.Muda mfupi baada ya Mike kuziachia mbegu zake za kiume, Bi harusi alipatwa na maumivu makali sana ambayo mwenyewe anayaelezea kuwa ni sawa na kama mtu alikuwa akipigilia misumari ndani ya mwili wake.Maumivu hayo yaliyoambatana na vipele yaliendelea kwa wiki kadhaa kabla ya kutoweka.Baada ya vipimo kadhaa vya madaktari iligundulika kuwa Julie ana aleji na mbegu za kiume za Mike.Madaktari walisema kwamba mwili wa Julie huzichukulia mbegu za kiume za Mike kama protini ambazo hazikubaliki kwenye mwili wake na hivyo kuufanya mwili wake kuzishambulia mbegu hizo za kiume.Hali aliyo nayo Julie imewafanya wanandoa hao wapya waghairi mpango wao wa kupata mtoto kwasababu uwezekano wa Julie kushika ujauzito ni finyu kwa kuwa mwili wake huzishambulia na kuziua mbegu za kiume kila zinapoingia kwenye mwili wake.Mike na Julie walianza mapenzi yao wakati wakiwa chuo kikuu na walivalishana pete za uchumba miaka miwili baadae na mwishoe mwaka 2005 waliamua kufunga ndoa.Lakini baada ya sherehe za kuisha na walipotaka kulila tunda kwa mara ya kwanza bila ya kutumia kondomu wakiwa kama mke na mume , usiku wa harusi ulibadilika ghafla na kuwa usiku wa majonzi."Kabla ya kuoana tulikuwa makini na tulitumia kondomu wakati wote, siku ya harusi hatukutaka kutumia kondomu", alisema Julie."Kwakuwa tulikuwa tumeishafunga ndoa hatukuona sababu ya kuogopa kupata ujauzito"."Na ndipo nilipopatwa na maumivu makali sana kama vile mtu ananichoma moto muda mfupi baada ya Mike kuniachia mbegu zake za kiume", aliendelea kusema Julie."Hali ilikuwa inatisha sana, maumivu yaliendelea kunisumbua kwa wiki kadhaa".Baada ya njia mbali mbali za kutibu tatizo hilo, zote kufeli, wanandoa hao wapya kwa kujua kuwa hawana uwezo wa kupata mtoto, wameanza taratibu za kutafuta mtoto watakayejitolea kumlea kama mtoto wao.Mkasa wa maisha yao umetengenezewa documentary na televisheni ya Discovery Channel na documentary hiyo iliyopewa jina la "Strange Sex" itarushwa hewani nchini Marekani wiki hii.

Tanzania Yabamizwa 5-1 na Misri


Timu ya soka ya taifa ya Tanzania imeshindwa kuwika nchini Misri na kukubali kipigo cha mabao 5-1.

Hadi mapumziko Taifa Stars ilikuwa imeishacharangwa 4-1 na ilipoingia kipindi cha pili iliongezwa goli jingine moja kufanya jumla ya magoli yaliyotinga kwenye nyavu za Tanzania kufikia matano

Wednesday, November 4, 2009

REPRESETING AFRICA


pecially his motherland, Tanzania in this year’s edition of the BET Hip Hop Awards, which was broadcasted on October 27 on BET (Black Entertainment Television) in the USA.


When asked by Emcee Africa presenter Lee Kasumba about his experience of recording the Cypher segment as some of you saw it during the broadcast Gsan had this to say:


“Well, the Cypher segment was recorded in New York before the actual award ceremony. For me, it was just amazing to be there with people like Eminem, KRS One, DJ Premier playing the beats, and being able to showcase what I had. Many people were blown away with what I did and asked me why I rhymed in Swahili ’cause they wanted to understand. I was just like ‘English is not my first language, I speak it, I love it but you will be able to mess me up if I rhyme in English’. There were emcees from all over the world in one setting, and I was happy to represent for Africa. I wasn’t starstruck, just glad to showcase what I did and could do with my American counterparts. I mean, think of it, we really have the same names, just one word changes, African American and African, do you understand what that means
GSAN(middle) with KRS ONE(right) and DJ Premier(left) in New York City.


BC SALUTES YOU GSAN and the entire X-Plastaz crew

Bia ya Kilimanjaro yamzindua DC Same!!



Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahimu Marwa (kushoto) akimkabidhi bendera ya taifa mwanariaadha, Francis Naali kabla ya kuanza kwa mbio maalumu za kukimbia mbio maalum za kukimbiza bendera ya taifa hadi kilele cha mlima kilimanjaro.Mbio zenye ujumbe wa “Fikisha Tanzani katika hatua ya juu zaidi” na kudhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro.
Mwanariadhaa, Francis Naali akianza mbio maalum za kukimbiza bendera ya taifa hadi katika kilele cha mlima kilimanjaro. Mbio hizo zilianza jana wilayani same huku zikiwa na ujumbewa "Fikisha Tanzania katika hatua ya juu zaidi" zimedhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya kilimanjaro.

Na Mwandishi Wetu, Same

MAPOKEZI makubwa ya wanariadha wanaokimbiza bendera ya Taifa kwenda kilele cha Mlima Kilimanjaro, yamemzindua Mkuu wa Wilaya ya Same, Ibrahim Marwa na sasa ameahidi kuelekeza nguvu zake katika kukuza mchezo huo wilayani mwake.
Marwa aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa anakabidhi bendera ya Taifa kwa mwanariadha nyota Francis Naali, aliyeanzisha ngwe ya mwisho ya mbio hizo zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.
Naali alikuwa anaanzisha mbio kumalizia kilomita 104 kati ya 567 walizokimbia wanariadha zaidi ya 70 tangu kuanza kwa mbio hizo Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam na kuendelea kwa siku nne mfululizo, zikipita katika mikoa ya Pwani, Tanga na hatimaye Kilimanjaro.
“Jamani, nimehamasika sana na ninawashukuru Bia ya Kilimanjaro kwa kuipa Same heshima ya kuwa na kituo cha mbio hizi. Binafsi nimehamasika na ninatangaza rasmi kwamba, kuanzia sasa nitaweka mkazo katika riadha wilayani kwangu.
wakiianza ngwe ya mwisho ya mbio hizo.
Naye Meneja Masoko wa TBL, David Minja akiwa mwenye tabasamu, alisema: “Tunajivunia kampeni hii ya kupandisha bendera katika Mlima Kilimanjaro, na kikubwa tunashukuru kwa jinsi Watanzania walivyopokea kampeni hii ya “Fikisha Tanzania Katika Hatua za Juu”. Tunajivunia mlima mrefu kuliko yote Afrika na tunajivunia bia yetu ya Kilimanjaro…”
Kauli ya shukrani kwa wakazi wa mikoa waliyopitia wanariadha hao ilitolewa pia na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Alisema; “Leo ni siku ya nne ya mbio hizi za aina yake na tunashukuru kwa mwamko ambao Watanzania wameuonyesha kote tulikopita.Sisi wa Bia ya Kilimanjaro tuko kamili na tunajipanga kuhakikisha mbio hizi zinapata mafanikio zaidi na zaidi, lengo likiwa kwenda sambamba na umaarufu wa mlima wa Kilimanjaro.”
Bia hiyo, ndiyo inayozidhamini klabu kongwe na maarufu zaidi katika soka nchini, Simba na Yanga, pia ni mdhamini wa muda mrefu wa mbio za kimataifa za Marathoni za Kilimanjaro na zile zinazoshirikisha wanariadha kutoka zaidi ya nchi 25 duniani.
Pia ni wadhamini wa Tuzo za Muziki za Kilimanjaro. Imekuwa pia ikidhamini michuano ya mpira wa kikapu ya mkoani Dar es Salaam `RBA Kili’.
Mbio hizo zilitarajiwa kuingia Marangu jana jioni, tayari kwa kuipandisha kileleni mwa Mlima Kilimanjaro, leo.

ALOGWA KWA KUTEMBEA NA MKE WA MTU


Kumbe huko Zambia kuna dawa kali za kienyeji. Huyo jamaa alitembea na mke wa mtu huko Zambia. Kafumaniwa na mume wa mwanamke wake. Huyo mume kaenda kumfanyia dawa kali. Jamaa kafaa baada ya ume wake kuvimba kuwa saizi ya paja! Bofya picha kusoma habari kamili. (Picha kutoka Michuzi Blog)