Friday, August 21, 2009

Askofu Anthony Mayala Afariki


Habari zilizoifikia blogu hii ya jamii kutoka Mwanza zinasema Archbishop Anthony Mayala wa Kanisa Katoliki Mwanza amefariki dunia leo katika Hospitali ya Bugando baada ya kuugua Ugonjwa wa moyo. Aidha chanzo hicho kinaeleza kuwa Askofu Mayala alikuwa safarini Sirari kikazi na kuzidiwa asubuhi ya leo na kukimbizwa Bugando kwa matibabu hadi mauti yalipomkuta. Bwana Alitoa na Bwana ametwaa Jina la Mungu lihimidiwe. Tunaungana na familia na Jumuia nzima ya Kanisa Katoliki kuwapa pole wafiwa

No comments:

Post a Comment